Instagram Yasherekea Miaka 10 kwa Maujanja Haya
Miaka 10 iliyopita tarehe 6 October mtandao maarufu wa Instagram ulizaliwa rasmi, hiyo inafanya mwaka huu 2020, Instagram kusherekea miaka 10 ya kuunganisha watu na biashara mbalimbali kote duniani. Katika kusherekea mia…
Miaka 10 iliyopita tarehe 6 October mtandao maarufu wa Instagram ulizaliwa rasmi, hiyo inafanya mwaka huu 2020, Instagram kusherekea miaka 10 ya kuunganisha watu na biashara mbalimbali kote duniani.
Katika kusherekea miaka hiyo 10, kwa mwezi huu October instagram imekuja na maujanja yaliyojificha ambapo unaweza kubadilisha Icon ya Instagram kupitia ndani ya app hiyo moja kwa moja. Unaweza kuchagua Icon mbalimbali ikiwa pamoja na Icon zilizotumika kwenye mtandao huo kwenye miaka ya mwanzoni wakati mtandao huo ulipo zaliwa kwa mara ya kwanza.
Unaweza kuangalia video hapo chini ili kujua jinsi ya kubadilisha Icon kwenye app yako ya Instagram kwa urahisi na haraka.
