WhatsApp Yaongeza Photo Filter na Albums Kwenye Mfumo wa iOS
Kama wewe ni mtumiaji wa simu zenye mfumo wa iOS basi hii ni habari njema kwako kwani hapo jana WhatsApp ilianza kutoa toleo lake jipya lenye sehemu mpya ndogo, sehemu hizo ni Photo Filter pamoja na Albums. Kwa upande wa…
Kama wewe ni mtumiaji wa simu zenye mfumo wa iOS basi hii ni habari njema kwako kwani hapo jana WhatsApp ilianza kutoa toleo lake jipya lenye sehemu mpya ndogo, sehemu hizo ni Photo Filter pamoja na Albums.
Kwa upande wa sehemu ya album sasa utakuwa ukituma picha zaidi ya tano picha hizo zitajiweka kwenye mfumo wa album ili kukupa urahisi na nafasi ya kujua picha hizo zilitumwa kwa pamoja. Pale utakapo gusa picha moja ndipo itaweza kujaa kabisa kuwa picha moja.
Pia kwa jinsi inavyonekana whatsapp inataka kuwekwa kama facebook kwani sasa WhatsApp imeongezwa sehemu ya filter kwenye sehemu ya kamera, kwa sasa ziko filter za aina tano lakini inategemewa filter hizo kuongezwa kadri siku zinavyokwenda, filter hizo zinafanyakazi kwenye video, Gif na hata kwenye picha.
