Kutumia App ya WhatsApp kwa Lugha ya Kiswahili

Amani JosephMarch 3, 20231 min read Programu ya WhatsApp ni moja kati ya programu zinazotumiwa na watu wengi sana kwa sasa, programu hii imewezesha watu kuwasiliana kwa urahisi, iwe ni watu kutoka nje au ndani ya Afrika.…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
March 3, 2023
1 min read

Programu ya WhatsApp ni moja kati ya programu zinazotumiwa na watu wengi sana kwa sasa, programu hii imewezesha watu kuwasiliana kwa urahisi, iwe ni watu kutoka nje au ndani ya Afrika.

Kurahisisha mawasiliano zaidi hivi karibuni mitandao mbalimbali ya kijamii imeanza kutambua Kiswahili kama lugha rasmi ya kuwasiliana ndani ya mitandao hiyo.

Kupitia programu ya WhatsApp ya Android sasa unaweza kubadilisha lugha ya programu hiyo moja kwa moja na utaweza kutumia programu hiyo ikiwa kwenye lugha adhimu ya kiswahili.

Kama unavyona kwenye picha hapo chini maneno yote kwenye programu hiyo yamebadilika na kuwa kwa lugha ya Kiswahili.

  • Jinsi ya Badilisha App ya WhatsApp Kuwa ya Kiswahili

Kama ulikuwa unataka kubadilisha programu yako ya WhatsApp ya Android kuwa ya kiswahili unaweza kufuata hatua hizi.

Kwanza hakikisha una update app yako ya WhatsApp kisha baada ya hapo fungua App hiyo kisha ingia kwenye Settings kisha chagua Chats.

Baada ya hapo moja kwa moja chagua sehemu ya App Language inayo patikana chini ya chat settings.

Kupitia sehemu hiyo bofya kuweza kubadilisha lugha ya programu ya WhatsApp na chagua Kiswahili.

Kwa kufanya hivyo programu ya WhatsApp itakuwa imebadilika na kuwa kwenye lugha ya Kiswahili.

Kwa kuwa lugha fasaha ya kiswahili ni ngumu kama unataka kurudisha WhatsApp kuwa lugha ya English basi unaweza kufanya hivyo kwa kuchagua sehemu ya Mpangilio > Soga > Lugha ya programu, badilisha na weka Lugha ya simu.

Kwa kufuata hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kubadilisha lugha ya programu yako ya WhatsApp kuwa Kiswahili. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuchat kupitia kwenye programu ya WhatsApp huku ukitembea.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Jinsi ya Kupata Bidhaa za Amazon Bure Bila Kulipia
March 2, 2023
2 min read
Next Post

Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)

March 4, 2023
3 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Jinsi ya Kuwezesha Dira ya Kisasa (Compass) Kwenye Simu
March 7, 2023
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuchukua Screenshot Kwenye Kompyuta
March 6, 2023
2 min read
  • Maujanja
Njia Rahisi ya Kuzuia Bando Kuisha Haraka (Android)
March 4, 2023
3 min read

Related guides

Related gadgets