WhatsApp Kuja na Njia Mpya ya Kuzuia Kusambaza Meseji za Uzushi
WhatsApp imekuwa akifanyiwa maboresho mbalimbali ili kufanya programu hiyo kuwa bora zaidi, hivi karibuni njia mpya kabisa inakuja ambayo itasaidia kuzuia kusambaza meseji za uzushi kupitia programu za WhatsApp. Kwa muji…
WhatsApp imekuwa akifanyiwa maboresho mbalimbali ili kufanya programu hiyo kuwa bora zaidi, hivi karibuni njia mpya kabisa inakuja ambayo itasaidia kuzuia kusambaza meseji za uzushi kupitia programu za WhatsApp.
Kwa mujibu wa tovuti ya WABetaInfo, sehemu hiyo mpya inaweza kutoa ujumbe kama meseji unayotaka kumtumia mtu imeshatumwa mara nyingi, Yani hapa nazungumzia zile meseji ambazo hutumika na watu na kukwambia uzitume kwa watu wengine 10 au zaidi.
Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo ujumbe huu utatokea kwa aliye tuma meseji hiyo na kama utamtumia mtu nae pia ataona ujumbe huo, kwa sasa bado hakuna habari kamili kama sehemu hii itakuja lini kwenye programu za WhatsApp lakini habari kutoka tovuti hiyo zinasema kwa sasa WhatsApp inafanya majaribio ya sehemu hiyo.
