WhatsApp Kuja na Njia Mpya ya Kurekodi Meseji za Sauti
Toka WhatsApp ilipo toa sehemu ya Voice messages hapo mwaka 2013, haijawahi kufanyiwa maboresho yoyote makubwa hadi kufikia sasa. Habari kutoka kwenye tovuti ya WABetaInfo zinasema kuwa WhatsApp inategemea kuboresha sehe…
Toka WhatsApp ilipo toa sehemu ya Voice messages hapo mwaka 2013, haijawahi kufanyiwa maboresho yoyote makubwa hadi kufikia sasa. Habari kutoka kwenye tovuti ya WABetaInfo zinasema kuwa WhatsApp inategemea kuboresha sehemu ya kurekodi sauti hasa kwenye mfumo mzima wa jinsi ya kurekodi sauti.
Maboresho hayo ni kuwa sasa utakuwa huna haja ya kushikilia kitufe cha kurekodi ili uweze kurekodi meseji za sauti, bali sasa baada ya kubofya kitufe cha kurekodi kwa sekude chake utaweza kuendelea kurekodi bila kushikilia kitufe cha kurekodi kwa kubofya huku unasogeza kitufe kipya ambacho kitaweza kufanya mtu aendelee kurekodi bila kushilia kwenye kitufe cha kurekodi.
WhatsApp inategemea kufanya mamboresho ya jinsi ya kurekodi meseji za sauti kwa kuleta kitufe kipya ambacho kitawezesha mtu kuendelea kurekodi meseji bila kushikilia kitufe cha kurekodi. pic.twitter.com/5XQD4FxSV2
— VinkoWeb (@VinkoWeb) November 16, 2017
Kizuri kuhusu ujio wa sehemu hiyo ni kuwa baada ya kuweza kubofya kitufe hicho ambacho kitakuwezesha kuendelea kurekodi, utaweza kuendelea kupitia baadhi ya meseji kwenye chat uliyopo angalia video hapo chini.
