Tetesi : WhatsApp Kuja na Programu Mpya Kwaajili ya Kompyuta
WhatsApp ni moja kati ya programu bora za kuchati zinazotumiwa na watu wengi zaidi duniani, hadi mwezi wa nne mwaka huu 2019 programu hiyo imefikisha watumiaji zaidi ya bilioni 1.6 kwa mwezi, huku india ikiwa inashikilia…
WhatsApp ni moja kati ya programu bora za kuchati zinazotumiwa na watu wengi zaidi duniani, hadi mwezi wa nne mwaka huu 2019 programu hiyo imefikisha watumiaji zaidi ya bilioni 1.6 kwa mwezi, huku india ikiwa inashikilia namba moja kwa kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 400.
Katika kuendeleza kujuhudi za kufanya programu hiyo kutumiwa zaidi, hivi karibuni tetesi zimeibuka zikidai kuwa WhatsApp inafanya maandalizi ya kuja na programu mpya ya WhasApp kwaajili ya Kompyuta. Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya WABetaInfo, Programu hiyo mpya ni tofauti kabisa na programu ya sasa ambayo nilazima simu yako iwe hewani ndipo uweze kuitumia.
And yes, in according to my rumor, UWP + the new multi platform system = you can use WhatsApp UWP on your PC if your phone (Android, iOS or Windows Phone) is off. https://t.co/PgNZTnOxlj
— WABetaInfo (@WABetaInfo) July 26, 2019
Kwa mujibu wa ripoti hiyo inasemekana programu hiyo mpya kwaajili ya kompyuta itakuwa na uwezo wa kutumiwa bila kuunganisha simu, hivyo kuruhusu watu kuweza kuchat kwa kutumia kompyuta bila kuunganisha na simu kama ilivyo kwenye programu ya sasa.
