Viber Kuongeza Sehemu Mpya ya Meseji Zinazojifuta Zenyewe

Unaweza ukawa huijui au hujawahi kujaribu kutumia programu ya Viber, hii ni programu ya kuchat kama ilivyo WhatsApp ambayo kwa sasa ina watumiaji takriban milioni 800 duniani kote. Programu hii inaongoza sana kutumika kw…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Unaweza ukawa huijui au hujawahi kujaribu kutumia programu ya Viber, hii ni programu ya kuchat kama ilivyo WhatsApp ambayo kwa sasa ina watumiaji takriban milioni 800 duniani kote. Programu hii inaongoza sana kutumika kwa nchi za Asia, Eastern Europe pamoja na Northern Africa.

Sasa katika kuhakikisha watumiaji wake wote wanapata kutumia programu hiyo kwa raha na kwa usalama programu hiyo inakuja na sehemu mpya inayoitwa “secret chat”. Sehemu hii itakuwezesha kutumia programu hiyo uku vitu unavyo chat vikiwa na uwezo wa kufutika ndani ya muda maalum (self destruct), sehemu hiyo inakuja baada ya kampuni hiyo kuleta sehemu mpya ya kukuwezesha kuweka password kwenye meseji zako ambazo unachat.

Viber kwa sasa inajitahidi kuongeza sehemu mpya ili kuweza kuvutia watumiaji wengi kutumia programu hiyo ambayo iko kwenye mfumo wa Android pamoja na iOS, unaweza kupakua programu hiyo sasa uweze kujaribu kupitia Play Store pamoja na App Store.

Related guides

Related gadgets