Hivi Karibuni Utaweza Kuunganisha WhatsApp na Instagram
Tokea mwaka 2012 Facebook iliponunua mtandao wa Instagram kwa dollar za marekani bilioni $1 sawa na zaidi ya Tsh Trilioni 2.2. Facebook imekua na jitihada kubwa kuhakikisha mtandao huo unaunganishwa na programu nyingine…
Tokea mwaka 2012 Facebook iliponunua mtandao wa Instagram kwa dollar za marekani bilioni $1 sawa na zaidi ya Tsh Trilioni 2.2. Facebook imekua na jitihada kubwa kuhakikisha mtandao huo unaunganishwa na programu nyingine kutoka kampuni ya Facebook.
Kuonyesha hilo, hivi leo habari kutoka kwenye mitandao mbalimbali ya Habari za teknolojia zinasema kuwa, Facebook ambayo ndio kampuni miliki ya programu za WhatsApp na Instagram imepanga kuleta sehemu mpya ambayo itakuwa inakuwezesha kuunganisha akaunti yako ya Instagram pamoja na namba yako ya WhatsApp.
Kupitia mtandao wa Wabetainfo ambao unatoa habari mbalimbali kuhusu ujio wa sehemu mpya kwenye programu ya WhatsApp, hivi leo umeandika kuwa sehemu hiyo inaonekana kuwepo kwenye hatua za majaribio na siku sio nyingi huenda sehemu hiyo ikaja rasmi kwanza kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp ya biashara.
https://twitter.com/theinformertz/status/1052968608748490752
Kupitia sehemu hiyo mpya watumiaji wa programu ya WhatsApp ya biashara watakuwa na urahisi wa kuweza kuwa onyesha wafuatiliaji wao akaunti zao za Instagram pia njia hii italeta urahisi kwa Instagram kuweza kufanya Verification ya kurasa mbalimbali za mtandao wa Instagram.
Kwa sasa kama nilivyosema sehemu hii iko kwenye hatu za majaribio hivyo siku sio nyingi tutasikia mengine mengi kuhusu sehemu hiyo mpya.
