Sasa Utaweza Kutuma Pesa Kwenye Programu ya Gmail ya Android
Tayari unauwezo wa kutuma ujumbe mfupi, picha na file mbalimbali kwa kutumia prgramu ya gmail lakini je unaonaje sasa ukiweza kutuma pesa kwa kutumia programu yako ya Gmail ya mfumo wa Android.? Google kupitia programu y…
Tayari unauwezo wa kutuma ujumbe mfupi, picha na file mbalimbali kwa kutumia prgramu ya gmail lakini je unaonaje sasa ukiweza kutuma pesa kwa kutumia programu yako ya Gmail ya mfumo wa Android.?
Google kupitia programu yake ya Gmail ya mfumo wa Android sasa inakuwezesha kutuma pesa kwa kutumia programu yako ya gmail. Google inakuwezesha kufanya yote hayo kwa kuunganisha na huduma ya Google Wallet ambapo ndio itakuwezesha kutuma pesa pale unapotaka kutuma barua pepe yako.
Kwa sasa huduma hii haipatikani kwa tanzania lakini inategemewa kuja kwenye siku za usoni hivyo endelea kutumia programu yako ya Gmail uku ukitembelea VinkoWeb kila siku ili kupata habari za sehemu hiyo mpya pindi itakapo kuja kwa hapa Tanzania.
