Tovuti za Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi

Amani JosephJune 28, 20222 min read Ni wazi kuwa Android ni moja ya mfumo maarufu sana hivi sasa, mwaka 2017 mfumo huu ulishikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa mfumo unaotumiwa zaidi duniani, huku soko la Play Store kwa kip…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20263 min read
Amani Joseph
June 28, 2022
2 min read

Ni wazi kuwa Android ni moja ya mfumo maarufu sana hivi sasa, mwaka 2017 mfumo huu ulishikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa mfumo unaotumiwa zaidi duniani, huku soko la Play Store kwa kipindi hicho likiwa na idadi ya Apps zaidi ya milioni 2 hapo mwezi march mwaka 2022.

Sasa kutokana na umaharufu wa mfumo huu ni wazi kuwa watu wengi wamekuwa wakitaka kutengeneza Android apps kuliko hata app za mifumo mingine, sasa kama wewe ni mmoja wa watu waliokuwa wanataka kutengeneza Android app kwa ajili ya tovuti yako basi makala hii ni kwa ajili yako.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia tovuti mbalimbali ambazo zitakusaidia kutengeneza App kupitia tovuti hizo bila kuwa na ujuzi wowote na bila kutumia gharama yoyote. Kumbuka tu baadhi ya tovuti hizi zinahitaji malipo ili kutoa baadhi ya huduma ila unaweza kutengeneza apps bila hata kuwa na huduma hizo, basi baada ya kusema hayo twende moja kwa moja tukangalie tovuti hizi.

TABLE OF CONTENTS

  • 1. Andromo
  • 2. Mobincube
  • 3. Appypie
  • 4. Appsgeyser

Andromo

Kama wewe ni somaji wa tovuti ya VinkoWeb basi tovuti hii sio ngeni kwako, Andromo ni tovuti ambayo tayari tulisha weza kuonyesha jinsi ya kutumia na kutengeneza app za Android kwa urahisi, kama unataka kujua jinsi ya kutumia basi unaweza kusoma makala nzima hapa. Mbali na hayo Andromo haina tofauti sana na tovuti iliyopita kwani unahitaji kuwa na barua pepe ili kupokea app pale inapo malizika kutengenezwa.

Tembelea Tovuti Hapa

Mobincube

Mobincube ni tovuti nyingine nzuri ya kukusaidia kutengeneza apps za Android bila kuwa na ujuzi wowote, tovuti hii ni nzuri sana na inaweza kukusaidia kutengeneza app kwa haraka na rahisi. Kama ilivyo tovuti zingine kwenye list hii pia unahitaji kuwa na email ili kuweza kutumia tovuti hii kwa urahisi na haraka.

Tembelea Tovuti Hapa

Appypie


Appypie ni tovuti nyingine ambayo nahisi watu wengi watakuwa wanafahamu, tovuti hii ni bora sana kwa sababu inakupa uwezo wa kutengeneza app nzuri sana. Tofauti ya tovuti hii na nyingine kwa list hii ni kuwa appypie inatengeneza apps ambazo zinakuja na matangazo ambayo ili kuondoa matangazo hayo ni lazima kulipia kiasi kidogo. Andromo pia inakuja na sehemu kama hii.

Tembelea Tovuti Hapa

Appsgeyser

Appsgeyser ni tovuti nyingine bora sana ya kutengeneza apps za Android, tovuti hii ni nzuri sana kwa sababu inakusaidia kutengeneza apps ambazo unaweza kuweka matangazo na kupata pesa kutokana na app yako. Tovuti hii ni rahisi sana kutuia na ukweli inafanya kazi vizuri sana, ili kutumia tovuti hii unahitaji barua pepe ili kuweza kutumia kwa urahisi na haraka.

Tembelea Tovuti Hapa

Na hizo ndio baadhi tu ya tovuti ambazo unaweza kutumia kutengeneza Apps za Android, kumbuka unaweza kutengeneza app kwa kutumia tovuti hizo bure kabisa na pia kuna baadhi ya tovuti hapa ambazo unaweza kulipia ili kupata sehemu nyingi zaidi kwenye app yako, lakini pia unaweza kuchagua kutumia tovuti hizi bure kabisa.

Kama unataka kujifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza app ya Android unaweza kuangalia video hapo chini au pia unaweza kubofya hapa kusoma makala nzima jinsi ya kutengeneza app bila kuwa na ujuzi wowote na kwa kutumia simu ya Android.

Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya VinkoWeb kila siku ili kuendelea kujifunza njia mbalimbali za kutumia teknolojia.

  • Programu Mpya
Updated:
Previous Post
Hizi Hapa Movie Nzuri za Kuangalia Jumapili #1
June 26, 2022
1 min read
Next Post

Best Tecno Smartphones in Tanzania (2026 Updated)

June 29, 2022
1 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Fahamu Mambo Haya Muhimu Kuhusu Password Yako
July 12, 2022
4 min read
  • Maujanja
Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono
July 5, 2022
2 min read
  • Maujanja
  • Programu
Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake
July 2, 2022
2 min read

Related guides