TCRA Yafafanua Usajili wa Laini kwa Kutumia Alama za Vidole
Hivi karibuni taarifa kutoka kwenye mitandao ya simu zilibainisha kuwa, sasa kutakuwepo na aina mpya ya usajili wa laini za simu za mkononi ambao utahusisha alama za vidole. Aidha katika taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikito…
Hivi karibuni taarifa kutoka kwenye mitandao ya simu zilibainisha kuwa, sasa kutakuwepo na aina mpya ya usajili wa laini za simu za mkononi ambao utahusisha alama za vidole.
Aidha katika taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikitolewa na mitandao mbambali ya simu kupitia meseji za ujumbe mfupi, kumekuwa na maswali mengi sana na wengi wakiwa wanataka kujua juu ya utaratibu mzima wa usajili huo utakavyokuwa.
Sasa hivi leo taarifa kupitia tovuti ya mwananchi zinasema kuwa Kaimu meneja mawasiliano kwa umma wa mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania TCRA, Semu Mwakyanjala alisema walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa hivyo watoa huduma za simu za mkononi wame ruhisiwa kuanza kutumia.
Hata hivyo meneja huyo alisema kuwa mfumo huo unaotumia alama za vidole na picha ni wenye uhakika na ambao ni vigumu mtu kughushi. “Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi,” alisema kaimu meneja huyo wa TCRA.
Katika kupata ufafanuzi wa jinsi usajili huo utakavyo kuwa, mwandishi wa tovuti ya mwananchi ali-wasiliana na meneja uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando ambaye alimwambia mwandishi huyo kuwa, Airtel itanza kufanya usajili huo mpya kwa hatua ya majaribio hivi karibuni.
Meneja huyo wa Airtel Tanzania aliendelea kusema, kupitia mpango huo wa majaribio wataanza kusajili katika mikoa minne ya Dar es Salaam, Pwani, Iringa na Singida. Pia, uta fanyika Zanzibar na kote huko usajili huo utafanyika kwa awamu hiyo kwa wateja wapya.
Meneja huyo aliendelea kuongeza kuwa, baada ya hatua hiyo kukamilika kampuni hiyo itaendelea na kuwasajili watu wengine hata ambao walisha sajiliwa awali kwa nia ya kuboresha zaidi mfumo huo.
