Programu ya Siri Kuweza Kusoma Kwa Sauti Meseji za WhatsApp
Watumiaji wa simu za iphone sasa wanaweza kufaidika na toleo jipya la programu ya Whatsapp kwani sasa programu ya siri imewezeshwa kusoma meseji zako za whatsapp kwa sauti. Katika toleo hilo jipya la Whatsapp watumiaji w…
Watumiaji wa simu za iphone sasa wanaweza kufaidika na toleo jipya la programu ya Whatsapp kwani sasa programu ya siri imewezeshwa kusoma meseji zako za whatsapp kwa sauti. Katika toleo hilo jipya la Whatsapp watumiaji wataweza kuwasha sehemu hiyo kupitia settings za programu ya Whatsapp.
Mtumiaji ataweza kuamuru siri kusoma meseji za whatsapp kwa kusema maneno ya “Hey Siri”, kumbuka ili kupata sehemu hii nilazima kuwasha shemu hiyo kupitia programu ya whatsapp kwa kwenda kwenye settings menu. Kwa kutumia sehemu hiyo mpya unaweza kujibu meseji pia kwa kusema kusema maneno na programu hiyo itakusaidia kuandika.
Kwa bahati mbaya kama wewe unatumia toleo la chini ya iOS 10.3 hutoweza kupata sehemu hiyo hivyo kama bado huja update simu yako ya iphone kwenda kwenye toleo jipya basi fanya hivyo kwa kudownload toleo jipya la iOS 10.3 sasa ili uweze ku-enjoy sehemu hiyo mpya.
