Sasa Chat na Share Video Moja kwa Moja Kwenye App ya YouTube
Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti yetu lazima utakuwa umesha soma makala iliyokuwa inagusia kuhusu kuja kwa sehemu ya kuchat na kushare video kwenye Youtube. Kama ulisha soma makala hiyo basi hii ni habari njema kwani s…
Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti yetu lazima utakuwa umesha soma makala iliyokuwa inagusia kuhusu kuja kwa sehemu ya kuchat na kushare video kwenye Youtube.
Kama ulisha soma makala hiyo basi hii ni habari njema kwani sasa sehemu hiyo imewezeshwa rasmi na Youtube na sasa utaweza kuchati na watu wengine huku mkiongelea video mbalimbali kupitia programu za youtube za iOS na Android.
https://www.youtube.com/watch?v=feBF_IY-HI8
Sehemu hiyo inapatikana kwenye app zote ikiwa imeandikwa share, kama bado ujaiona sehemu hiyo basi hakikisha una update programu yako ya Youtube na utaweza kuanza kuchati na kushiri video na watu mbalimbali kupitia mtandao wa Youtube.
UPDATE : Kama unataka kujifunza jinsi ya kutumia sehemu hii bofya hapa
Chanzo : Daily Mail
