Facebook Nayo Kuleta Sehemu Mpya ya Facebook Stories

Kwa muda sasa Facebook imekua ikifanya majaribio ya sehemu mpya ya Facebook Stories kwenye programu zake za Facebook Messenger za mifumo ya iOS pamoja na Android. Majaribio hayo yaliokua yakifanyika kwa watumiaji wa nchi…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Kwa muda sasa Facebook imekua ikifanya majaribio ya sehemu mpya ya Facebook Stories kwenye programu zake za Facebook Messenger za mifumo ya iOS pamoja na Android. Majaribio hayo yaliokua yakifanyika kwa watumiaji wa nchini Poland, sasa yameamia nchini Ireland hii ikiwa ni hatua za karibu za kuanza kusambaza kwa sehemu hiyo kwa watumiaji wote duniani.

Kwa mujibu wa tovuti ya Business Insider ya nchini marekani sehemu hiyo mpya itakuwa sawa na ile ya kwenye programu za Snapchat pamoja na Instagram. Kwa kutumia sehemu hiyo Stories zote zitatokea kwa juu kama vile kwenye programu ya instagram inavyokua, pia mtumiaji wa sehemu hiyo atawezeshwa kutuma storie yake ambayo haita onyeshwa kwenye sehemu ya timeline bali stories zote zitakuwa zikionekana kwenye sehemu hiyo maalum ya Facebook Stories.

Mpaka sasa bado haijajulikana tarehe halisi ya lini sehemu hiyo itanza kutoka kwenye programu zote za Facebook Messenger za iOS pamoja na Android, lakini dalili zinaonyesha watumiaji wa Facebook watapata sehemu hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.

Related guides

Related gadgets