Sasa Utaweza Kusave Video za Insta Live ili Kuangalia Baadae
Hivi karibuni mtandao wa Instagram ulileta sehemu mpya iliyowezesha watu kurekodi video live, sehemu hiyo ya Insta Live kwa sasa ni maarufu hasa hapa Tanzania lakini kulikua na tatizo moja tu ambalo sasa instagram wamepa…
Hivi karibuni mtandao wa Instagram ulileta sehemu mpya iliyowezesha watu kurekodi video live, sehemu hiyo ya Insta Live kwa sasa ni maarufu hasa hapa Tanzania lakini kulikua na tatizo moja tu ambalo sasa instagram wamepatia ufumbuzi.
Hivi karibuni instagram italeta uwezo wa kuhifadhi (save) video za live stream (Insta Live) mara baada ya kumaliza video yako, sehemu hiyo itakuwezesha kusave video yako kwenye simu yako na kama utataka utaweza kuipost tena kwenye mtandao wa instagram. Tofauti ni kwamba views na like hazitoweza kurekodiwa bali utaweza kupata video yenyewe tu.
Hata hivyo sehemu hiyo inawezeshwa kwa watu wenye video hizo hivyo usiwe na wasiwasi kuhusu mtu kuchukua video yako, sehemu hiyo inategemewa kuja hivi karibuni hivyo pale unapo ona kuna updates za programu hiyo hakikisha una update ili kuweza kupata sehemu hiyo mpya ambayo inapatikana mara baada ya kumaliza video yako ya kwenye mtandao huo.
