Sasa Utaweza Kufanya Ultra Sound kwa Kutumia Simu ya Mkononi
Kampuni inayo chipukia ya Butterfly Network, hivi karibuni imefanya ugunduzi wa kifaa kipya kinachoitwa iQ. Kifaa hichi kinauwezo mkubwa wa kumuwezesha daktari au mtu yoyote kuweza kufanya Ultra Sound kwa kutumia simu ya…
Kampuni inayo chipukia ya Butterfly Network, hivi karibuni imefanya ugunduzi wa kifaa kipya kinachoitwa iQ. Kifaa hichi kinauwezo mkubwa wa kumuwezesha daktari au mtu yoyote kuweza kufanya Ultra Sound kwa kutumia simu ya mkononi maarufu kama smartphone.
Kifaa hicho kidogo cha IQ ni kama vile umebeba maabara nzima kwenye kiganja cha mkono wako kwani kifaa hicho haki hitaji mtaalamu wa kukiendesha na badala yake unachotakiwa kufanya ni kukipachika kwenye simu yako ya iPhone na moja kwa moja utaweza kuanza kufanya ultra sound mwenyewe.
Wote tunajua kuwa vifa vya kawaida vya ultra sound vinatumia teknolojia ya compressed charged crystals au ceramics kuweza kutuma sauti ambayo baadae mwagwi wa sauti hiyo unapimwa kwa kutumia picha ambayo ndio inayo onekana kwenye kifaa cha ultra sound.
Lakini kwenye kifaa cha IQ teknolojia hiyo imebadilishwa na sasa kifaa hicho kitatumia teknolojia ya capacitive micromachine ultrasound transducers au (CMUT). Ambapo kifaa hicho kinakuwa na vimistari vidogo vyanye vitufe kama ngoma ambavyo hutoa mtetemeko kulingana na eneo inapo elekezwa na mtetemeko huo baadae kupimwa kwa kutumia mfumo maalum ambao hutumia data kuweza kutengeneza picha ambayo utaweza kuiona kwenye simu yako ya mkononi.
Japokua kifaa hicho hakina uwezo wa kuonyesha picha angavu kama zile za MRI au CT scan, lakini kifaa hicho kinauwezo mkubwa wa kupima sehemu mbalimbali zile ambazo haziitaji wewe kufika kwenye maabara kubwa ya kidaktari. Kwa sasa kifaa hicho kimeruhusiwa kutumika kwa madaktari tu huku jitihada zikiendelea kuwezesha kuhakikisha kinawafikia watumiaji wote wa majumbani.
