Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Amani JosephAugust 16, 20222 min read Mtandao wa Instagram hivi karibuni umefanya maboresho mbalimbali ikiwa pamoja na njia mpya ya kuficha views na likes ambapo watu hawatoweza kuona idadi ya views au like kwenye profil…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
August 16, 2022
2 min read

Mtandao wa Instagram hivi karibuni umefanya maboresho mbalimbali ikiwa pamoja na njia mpya ya kuficha views na likes ambapo watu hawatoweza kuona idadi ya views au like kwenye profile yako ya Instagram, Unaweza kuzuia watu kuona kwenye ukurasa wako mzima au kwenye picha moja moja.

Mbali na hayo, Instagram hivi karibuni pia ili tambulisha sehemu mpya ya kurudisha picha au video ambazo umezifuta kwenye akaunti yako, kupitia sehemu hiyo unaweza kurudisha picha au video za hadi siku 30 nyuma, yaani kama umefuta picha ndani ya siku 30 zilizopita basi utaweza kuirudisha moja kwa moja kwa kupitia njia hii.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kurudisha picha ambazo ulizifuta kwenye akaunti yako ya Instagram basi unasoma makala sahihi. Bila kuendelea kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye makala hii.

Rudisha Picha ulizofuta Instagram

Kwa kuanza hakikisha una sasisha au una-update app ya Instagram kupitia Play Store au App Store, baada ya ku-update app yako moja kwa moja endelea kwenye hatua zifuatazo.

Fungua profile yako ya Instagram kisha bofya sehemu ya Menu iliyopo upande wa kulia juu, mara nyingi sehemu hii huwa na vimikato vitatu vilivyopo kwa mlalo.

Baada ya hapo bofya sehemu ya Settings ambayo inapatikana mara baada ya kubofya Menu kwenye hatua iliyopita.

Baada ya hapo moja kwa moja bofya sehemu ya Account ambayo inapatikana mara baada ya kubofya sehemu ya Settings.

Baada ya hapo moja kwa moja kwenye ukurasa unaofuta ambao umefunguka baada ya kubofya Account, mwisho kabisa utaona sehemu mpya ya Recently Deleted, bofya hapo kuendelea kwenye hatua inayofuata.

Kwenye ukurasa unaofuata utaweza kuona picha au video ambazo umezifuata ndani ya muda mfupi wa siku 30 zilizopita.

Chagua picha au video unayotaka kuirudisha na moja kwa moja baada ya picha hiyo kufunguka endelea kwa kubofya vitufe vitatu vilivyopo juu upande wa kulia na moja kwa moja chagua sehemu ya Restore.

Kama unataka kuondoa picha hiyo kabisa unaweza kubofya sehemu ya Delete ambapo picha yako au video itafutika kabisa na hutoweza kuipata tena kupitia Instagram.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi
August 16, 2022
2 min read
Next Post

Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android

August 23, 2022
2 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
  • Programu
Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake
August 28, 2022
3 min read
  • Maujanja
  • Programu
Apps Nzuri za Android Kwaajili ya Kulinda Afya Yako
August 28, 2022
3 min read
  • Maujanja
Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android
August 23, 2022
2 min read

Related guides

Related gadgets