Wezesha (PIP) Picture in Picture Kwenye Video Yoyote (Chrome)

Amani JosephJanuary 30, 20242 min read Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kufanya kazi kwenye kompyuta yako huku unaangalia video basi makala hii ni kwaajili yako. Kupitia njia hii nitakuonyesha jinsi ya kuwezesh…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/July 5, 20262 min read
Amani Joseph
January 30, 2024
2 min read

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kufanya kazi kwenye kompyuta yako huku unaangalia video basi makala hii ni kwaajili yako. Kupitia njia hii nitakuonyesha jinsi ya kuwezesha PIP au Picture in Picture Mode kwenye video yoyote kupitia Chrome.

Kitu cha muhimu ni kuhakikisha kuwa unatumia browser kwenye kifaa chako hapa na maana computer (desktop au laptop) yenye kutumia mfumo wa Windows.

Kama tayari unayo yote hayo basi moja kwa moja utaweza kuendelea kwenye hatua inayofuata. Kwa kuanza unatakiwa kuona jinsi PIP au picture in picture inavyofanya kazi. Kwa mfano mimi wakati naandaa makala hii nimekuwa nikiangalia series kupitia Netflix huku nikiandika makala hii.

Kama unavyoweza kuona hapo juu unaweza kuangalia video bila kuwa umehama kwenye kazi au kitu unachofanya. Unaweza kuweka video juu ya kitu chochote iwe ni app kwenye kompyuta yako au sehemu yoyote ile ndani ya PC yako.

Basi baada ya kujua jinsi PIP inavyo onekana kwenye kompyuta yako basi moja kwa moja unaweza kuendelea kwenye hatua jinsi ya kuwezesha sehemu hii kwenye kompyuta yako.

Hatua ya kwanza, bofya hapo chini na utapelekwa kwenye extension store ambao unatakiwa kupakua na kuinstall extension. Bofya hapo chini kupakua moja kwa moja.

Baada ya hapo moja kwa moja unaweza kuendelea kwa kufuata hatua hapo chini na utaweza kuwezesha picture in piture kwenye browser yako ya chrome kupitia kompyuta. Sehemu hii inafanya kazi kwenye video yoyote iwe Netflix, Youtube au mtandao mwingine wowote.

Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu browser ya Chrome unaweza kusoma hapa kujua njia mpya mbalimbali za kutumia Chrome kwenye simu yako ya Android. Kwa maujanja zaidi hakikisha una tembelea VinkoWeb kila siku, pia pakua app yetu kupitia hapa. Usisahau kubadili lugha kwende kiswahili ili kupata makala zetu za kiswahili.

Updated:
Previous Post
Njia Bora ya Kudhibiti Matumizi ya Smartphone kwa Watoto
January 25, 2024
3 min read
Next Post

Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki

January 31, 2024
2 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Jinsi ya Kuzuia Apps Ku-update Zenyewe Kupitia Play Store
February 2, 2024
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kufuta Kwa Haraka Picha na Mafaili Yanayofanana
February 1, 2024
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuondoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki
January 31, 2024
2 min read

Related guides

Related gadgets