Jinsi ya Kutengeneza Muziki Kwa Maandishi Kwa Kutumia AI

Amani JosephJune 23, 20242 min read Katika ulimwengu wa AI ni wazi kuwa kila sehemu inatarajiwa au imeguswa na mabadiliko haya ya teknolojia. Moja kati ya mabadiliko hayo ni pamoja na mabadiliko ya jinsi muziki unavyo an…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
June 23, 2024
2 min read

Katika ulimwengu wa AI ni wazi kuwa kila sehemu inatarajiwa au imeguswa na mabadiliko haya ya teknolojia. Moja kati ya mabadiliko hayo ni pamoja na mabadiliko ya jinsi muziki unavyo andikwa na kutengenezwa.

Kampuni moja ambayo imejikita kwenye utengenezaji wa Muziki kupitia teknolojia ya AI imetengeneza mfumo ambao mtu yoyote anaweza kutumia kutengeneza muziki ambao unaweza kusikilizwa na mtu yoyote.

Udio ni mfumo mpya wa AI ambao unaweza kutengeneza muziki wenye uwezo mkubwa wa kutambuliwa kama umetengenezwa na binadamu japo kuwa ume tengenezwa na AI, Mfumo huu unaweza kutengeneza kuanzia Beat, Mdundo na hata maneno pia. Unaweza kusikiliza mfano wa kionjo hapo chini.

Uzuri wa mfumo huu unaweza kutengeneza muziki hata kwa lugha ya kiswahili na hata lugha nyingine za kigeni kama kiarabu na nyingine.

Jinsi ya Kutengeneza Muziki kwa AI

Kama umependa ulicho sikia na unataka kutengeneza muziki kama huu kwa kutumia AI basi unaeza kufuata hatua hizi rahisi.

Hakikisha unayo internet kwenye simu yako kisha moja kwa moja tembelea tovuti hapo chini na moja kwa moja tengeneza akaunti ya bure.

Tembelea Tovuti ya UDIO Hapa

Chagua Sign Up kisha chagua Google moja kwa moja utaweza kutengeneza akaunti kwa kutumia akaunti yako ya Google.

Baada ya hapo utapelekwa kwenye uwanja ambapo unatakiwa kuandika maelezo ya muziki unaotaka, unaweza kuandika kwa kingereza (English) huku ukitaka mfumo huu utengeneze nyimbo yenye mashairi ya kiswahili.

Kwa mfano mimi ili kupata nyimbo hiyo hapo juu niliandika prompt hii.

Prompt: Create a Bongo Flava song talks about Audio Mpya

Baada ya kuandika prompt yako vizuri subiri baada ya muda na moja kwa moja utaweza kupata mfano wa kwanza wa nyimbo unayotaka. Kama utakuwa umeridhika na sample ya kwanza unaweza kuongeza nyimbo hiyo kwa kubofya sehemu ya Extend.

Pia unaweza ku publish nyimbo yako Kwaajili ya watu wengine kusikiliza au unaweza kufanya remix ya nyimbo yoyote unayo iona kwenye platform ya Udio.

Pia usisahau kupakua app yetu ya VinkoWeb kupitia soko la Play Store kisha badilisha lugha kwa kubofya Menu alafu chagua Swahili Site.

Price: Free
Updated:
Previous Post
Infinix Note 40 Series Simu Yenye Teknolojia ya All Round Fastcharge 2.0
May 25, 2024
2 min read
Next Post

Jinsi ya Kutuma Mafile Kwa Haraka Android, iOS, Windows na Mac

August 4, 2024
2 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Download Video Instagram, Twitter, TikTok, na Mitandao Mingine
August 26, 2024
2 min read
  • Kompyuta
  • Maujanja
Mambo ya Kujua Kabla ya Kununua Laptop ya MacBook
August 22, 2024
5 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kutuma Mafile Kwa Haraka Android, iOS, Windows na Mac
August 4, 2024
2 min read

Related guides

Related gadgets