Jinsi ya Kuangalia Channel Zaidi ya 5000+ Kupitia Android TV

Amani JosephMay 24, 20232 min read Ni wazi kuwa kwa sasa smart TV zimekuwa zikipatikana kwa wingi sana hasa hapa Tanzania, mbali ya upatikanaji pia bei ya TV hizi pia imekuwa ni nafuu sana kutokana na wingi wa TV hizi. S…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
May 24, 2023
2 min read

Ni wazi kuwa kwa sasa smart TV zimekuwa zikipatikana kwa wingi sana hasa hapa Tanzania, mbali ya upatikanaji pia bei ya TV hizi pia imekuwa ni nafuu sana kutokana na wingi wa TV hizi.

Sasa kwa sababu ya hili ni wazi kuwa unaweza sasa kutumia Smart TV yako kama ilivyo simu yako ya Android, tukianza na njia hii ya jinsi ya kuangalia IPTV kupitia Smart TV yako yenye kutumia mfumo wa Android.

Kwa kuanza kama kawaida unatakiwa ku-download app ya IPTV kupitia link hapo chini, baada ya kudownload usijali nitaenda kuonyesha hatua nyingine za muhimu unazo takiwa kufanya.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii hakikisha una install kwenye TV yako, kama TV yako inayo browser unaweza kutembelea ukurasa huu kupitia TV yako na kudownload app hii moja kwa moja.

Baada ya hapo moja kwa moja tembelea ukurasa huu kisha bofya sehemu iliyo andikwa Copy Link au bofya hapo chini, kisha nakili link hiyo, kisha moja kwa moja fungua app ya IPTV kisha bofya sehemu ya Load Your Playlist or File/URL na kisha paste link hiyo kwenye sehemu hiyo.

Copy Link Hapa

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona channel zaidi ya 5000+ ambazo utaweza kuangalia moja kwa moja kupitia Smart TV yako ya Android. Kumbuka unatakiwa kuwa na Internet kwenye TV yako ili kuweza kuangalia channel hizi kwenye TV yako.

Kitu cha muhimu ni kuwa angalia channel hizi zipo nyingi sana kiasi kwamba sio channel zote zenye maadili hivyo hakikisha unakuwa makini unapo weka channel hizi kwenye TV yako ya sebuleni kwako, hasa kama kuna watoto.

Baada ya kusema hayo basi bila shaka umeweza kuangalia IPTV kupitia kwenye Smart TV yako, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kuzima bluetooth kwenye Smart TV yoyote inayotumia mfumo wa Android.

Updated:
Previous Post
Ongeza Uwezo wa Simu Yako Kupitia Apps Hizi za Android
May 15, 2023
3 min read
Next Post

Jinsi ya Kusajili Biashara Kupitia Google My Business (2026)

May 26, 2023
4 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller
June 1, 2023
2 min read
  • Maujanja
Rahisisha Mambo Mbalimbali kwa Kutumia Tovuti Hizi
May 30, 2023
3 min read

Related guides

Related gadgets