HyperDrive Kifaa cha Kuongeza Port Kwenye MacBook Pro

Kama tunavyojua MacBook Pro ya mwaka 2016 inakuja na aina mpya ya port ambazo hizi zinatofautiana sana na zile port za kawaida za USB ambazo tunazitumia kila siku. Kukosekana kwa port hizi kumefanya watumiaji wengi sana…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Kama tunavyojua MacBook Pro ya mwaka 2016 inakuja na aina mpya ya port ambazo hizi zinatofautiana sana na zile port za kawaida za USB ambazo tunazitumia kila siku. Kukosekana kwa port hizi kumefanya watumiaji wengi sana kuwa na vifaa vya kuunganisha (dongle) ili kutumia port hizo zilizo zoeleka.

Kutokana na ukosefu wa port hizo, matumizi ya vifaa hivyo yamekuwa makubwa sana ukizingatia MacBook hiyo ya mwaka 2016 haitumii kabisa port za kawaida au zilizo zoeleka. Ili kupunguza matumizi hayo ya vifaa vingi kampuni ya HYPER yenye makao makuu huko San Francisco, CA imegundua kifaa kipya kitanachoitwa HyperDrive.

https://www.youtube.com/watch?v=U5XlbCKQm1w

Kifaa hichi cha HyperDrive kina uwezo wa kufanya kompyuta yako ya MacBook Pro ya Mwaka 2016 kutumia port za kawaida za USB, HDMI na nyingine nyingi. Kwa sasa kifaa hichi kipo kwenye hatua za ambapo watengenezaji wake wanaomba msaada ili kumalizia kifaa hicho, kama unataka kutoa msaada unaweza kutembelea tovuti ya Kickstarter.com.

Kifaa hicho kwa sasa kinauzwa kwa dollar za marekani $49 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 110,000 lakini bei hiyo ni kupitia page yao iliyoko kwenye tovuti ya Kickstarter.com ambayo husaidia wajaria mali kupata msaada kutoka kwa watu mbalimbali ili kufanikisha kuingiza bidhaa zao sokoni.

Related guides

Related gadgets