Je Wajua: Hii Hapa Ndio Historia Fupi ya (#) Hashtag Ilipotoka

Wote tunaijua au tumesha itumia hashtag #, lakini ni wachache sana kati yetu tunaejua historia ya hashtag ilipo tokea kifupi ni kwamba hashtag imeanzia bali sana na kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kujua histori…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Wote tunaijua au tumesha itumia hashtag #, lakini ni wachache sana kati yetu tunaejua historia ya hashtag ilipo tokea kifupi ni kwamba hashtag imeanzia bali sana na kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kujua historia ya hashtag # basi ifuatayo ndio historia yake fupi.

Manamo mwaka 2007 mwezi August Chris Messina, mtaalamu wa mitandao ya kijamii aligundua hashtag ya kwanza ambayo ilikua ikitumika kwenye mtandao wa Twitter, hashtag hiyo ilikua maalum kwaajili ya kukusanya maongezi yote ambayo yalikua yakihusu kampuni iliyokuwa inaitwa Barcamp hashtag hiyo ilikua ni #barcamp.

Tukirudi nyuma kidogo hashtag ilikua ikitumika kwenye IRC au Internet Relay Chat mfumo wa zamani wa kuchati ulio kuwa ukitumiwa na makampuni mbalimbali. Kuhusu jina Hashtag lilipotoka bado historia nzima ya neno hilo haijawekwa wazi bali kwa mujibu wa tovuti mbali mbali mtandaoni neno hilo limetokana na neno “tag” na limegunduliwa na wagunduzi wa mtandao wa Twitter.

Na hiyo ndio historia fupi ya hashtag ilipotokea, bado historia hii haiakamilika kutokana na kuwa na makala mbalimbali zenye kusema tofauti uhalisia wa neno hilo ila ni uhakika hashtag ya kwanza ilianza kutumika hapo mwaka 2007 na ilitumiwa na Chris Messina kwenye mtandao wa Twitter na hiyo hapo chini ndio Tweet yenyewe.

https://twitter.com/chrismessina/status/223115412

Related guides

Related gadgets