Cheza Game Moja kwa Moja kwenye Facebook Messenger

Facebook hapo juzi ilitangaza kuwa kwa sasa ipo tayari kuachia game nyingine mpya ya PAC-MAN ambayo watumiaji wa Facebook Messenger wataweza kucheza game hiyo moja kwa moja kupitia programu hiyo yaani Facebook Messenger.…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Facebook hapo juzi ilitangaza kuwa kwa sasa ipo tayari kuachia game nyingine mpya ya PAC-MAN ambayo watumiaji wa Facebook Messenger wataweza kucheza game hiyo moja kwa moja kupitia programu hiyo yaani Facebook Messenger.

Game hiyo mpya inakuja moja kwa moja na uwezo wa kucheza game hiyo na nyingine nyingi kwenye programu hiyo kwa kubofya kitufe maalum, mtumiaji wa Facebook Messenger ataweza kucheza game hizo na marafiki na baadae kuonyesha kiasi cha point kwenye programu hiyo ili kuwezesha ushindani baina ya marafiki wanaotumia mtandao huo wa Facebook.

Game ambazo kwa sasa unaweza kucheza kupitia programu hiyo ya Facebook Messenger ni pamoja na Pac-Man, Space Invaders, Galaga na Words With Friends, ambazo zote hupatikana kwenye programu hiyo moja kwa moja. Kwa sasa sehemu hiyo mpya itapatikana kwenye toleo jipya la programu ya Facebook Messenger na sehem hiyo imepewa jina la Instant Games.

https://www.youtube.com/watch?v=qtNx1iQ1y00

Pia unaweza kucheza game hizo moja kwa moja kwenye sehemu ya News Feed, kumbuka pia kama bado hujapata toleo jipya la Facebook messenger download sasa kupitia Play Store au App Store ili kucheza game hizo.

Related guides

Related gadgets