Fanya Haya kwa Kugusa Sehemu ya Kamera Kwenye Simu Yako

Amani JosephSeptember 10, 20231 min read Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android njia hii inakuhusu, kupitia njia hii nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kubadilisha sehemu ya kamera ya mbele kuwa kitu…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
September 10, 2023
1 min read

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android njia hii inakuhusu, kupitia njia hii nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kubadilisha sehemu ya kamera ya mbele kuwa kitufe maalaum, yaani kama simu yako ina muonekano kama picha hapo chini basi njia hii ni kwaajili yako.

Haijalishi sehemu hiyo ya kamera ina kamera mbili au kamera mmoja bali kama kamera ya simu yako ipo ndani ya kioo njia hii itaenda kufanya kazi kwenye simu yako.

Sasa kitu cha muhimu ni kuhakikisha unapakua app kupitia link hapo chini, app hii itakusadia kuweza kubadilisha sehemu hiyo na kuruhusu sehemu hiyo kutumika kama kitufe maalum.

Yaani utaweza kuwasha kamera, kufungua app maalum, kuwasha tochi na mambo mengine mengi moja kwa moja kwa kugusa sehemu hii kwenye simu yako.

Pakua Toleo la Bila Kununua

Baada ya kupakua app hii moja kwa moja fungua app hii na kisha ruhusu app hii kwenye permission mbalimbali kisha utapelekwa kwenye uwanya wa Settings.

Unaweza kufanya mambo mbalimbali kama unaweza kuona kwenye video hapo chini, hakikisha unajaribu Menu mbalimbali ili kujua menu gani ni muhimu kwako.

Unaweza kufanya yote hayo kwa kubofya tu sehemu ya kamera kwenye simu yako. Kama kuna mahali umekwama unaweza kutuandikia kupitia maoni hapo chini, pia kwa unataka kujua maujanja zaidi unaweza kutembelea VinkoWeb kila siku.

Updated:
Previous Post
Namba Mbili Ndani ya Programu Moja ya WhatsApp!
September 8, 2023
2 min read
Next Post

Fuel Price in Tanzania (Bei ya Mafuta Tanzania) 2023

September 12, 2023
2 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Tumia Simu Iliyopasuka Kioo Kupitia Kompyuta
January 23, 2024
3 min read
  • Maujanja
  • Mitando Kijamii
Pakua Video Reels, Story, Picha za Instagram Bila App Yoyote
November 14, 2023
1 min read
  • Maujanja
Maujanja ya WhatsApp Hambayo Ulikuwa Hujui (2023)
November 13, 2023
4 min read

Related guides

Related gadgets