Facebook Yaleta Messenger Day Sehemu Nyingine Kutoka Snapchat

Hivi karibuni mtandao wa facebook umeleta sehemu mpya iitwayo Messenger Day, sehemu hii kama zilivyo baadhi ya sehemu mpya za mitandao ya instagram na facebook ni moja kati ya sehemu zilizo anzia kwenye mtandao wa kijami…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Hivi karibuni mtandao wa facebook umeleta sehemu mpya iitwayo Messenger Day, sehemu hii kama zilivyo baadhi ya sehemu mpya za mitandao ya instagram na facebook ni moja kati ya sehemu zilizo anzia kwenye mtandao wa kijamii ya Snapchat.

Sehemu hiyo kama ilivyokuwa kwenye programu ya Snapchat mtumiaji atapewa nafasi ya kuweka picha na video kupitia programu ya Facebook messenger na picha hizo au video zitapotea baada ya masaa 24. Sehemu hiyo mpya itakuruhusu kuweka urembo mbalimbali kwenye picha hizo kama vile maandishi yenye rangi mbalimbali, sticker na urembo mwingine unao patikana kwenye programu hiyo ya Facebook Messenger.

https://www.facebook.com/messenger/videos/1227636360689375/

Habari zinasema sehemu hii mpya ilianza kujaribiwa toka mwezi September, 2016 huko nchini Poland na sasa iko tayari kutoka kwa dunia nzima baada ya majaribio hayo ambayo yanaonekana yalienda vizuri. Sehemu hiyo kwa sasa inapatikana kwenye Facebook Messenger na kama bado hujaipati hakikisha una update programu yako ya Facebook Messenger ili kupata sehemu hiyo mpya.

Related guides

Related gadgets