Facebook Mfumo wa Kuzuia Picha Kutumika Zaidi ya Mara Moja

Kampuni ya Facebook hivi karibuni inatarajia kuzindua mfumo mpya ambao utaweza kuzuia watu au akaunti mbalimbali kutumia picha za watu wengine ambazo zina haki miliki (copyrighted). Mfumo huo mpya ambao utaweza kutumiwa…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Kampuni ya Facebook hivi karibuni inatarajia kuzindua mfumo mpya ambao utaweza kuzuia watu au akaunti mbalimbali kutumia picha za watu wengine ambazo zina haki miliki (copyrighted).

Mfumo huo mpya ambao utaweza kutumiwa na mtu yoyote, utaweza kusaidia watu kuzuia picha zao kutumika kwa kutuma maombi ya kuondoa picha hizo moja kwa moja kupitia facebook ambapo picha hizo zitaondolewa kwenye mitandao yote ya Facebook ikiwa pamoja na Instagram.

Sehemu hiyo mpya kwa sasa tayari imesha anza kutumika na kampuni mbalimbali ambazo facebook haijazionisha kwenye taarifa yake.

Kutumia sehemu hiyo mtumiaji anatakiwa kutuma file lenye format ya CSV, lenye maelezo yote ya haki miliki ya picha hiyo ikiwa pamoja na maelezo ya wapi haki miliki hiyo inatakiwa kuwekwa, yaani ni kwenye nchi gani ambapo unataka picha hiyo iweze kuondolewa.

Related guides

Related gadgets