Jinsi ya Kuwezesha Dira ya Kisasa (Compass) Kwenye Simu

Amani JosephMarch 7, 20232 min read Ni wazi kuwa simu za smartphone zimefanya mabadiliko makubwa sana, mabadiliko haya yamechangia sana kwenye maendeleo ya duniani kwa kuwa teknolojia imerahisha sana mambo. Pamoja na mam…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
March 7, 2023
2 min read

Ni wazi kuwa simu za smartphone zimefanya mabadiliko makubwa sana, mabadiliko haya yamechangia sana kwenye maendeleo ya duniani kwa kuwa teknolojia imerahisha sana mambo.

Pamoja na mambo mengi ambayo yamewezeshwa na teknolojia ya smartphone, pia kupitia smartphone yako unaweza kutumia dira au compass ya kisasa yenye uwezo mkubwa sana.

Kama wewe ni mtumiaji wa dira ni wazi kuwa ulishawahi kujaribu app mbalimbali kwenye simu yako, lakini kupitia makala hii nitakuonyesha njia bora kuliko zote za kuwezesha dira kwenye smartphone yako. Baadhi ya sehemu zinazoweza kupatikana kwenye njia hii ni pamoja na –

Utaweza kuwasha dira au compass ambayo inaweza kuonyesha ulipo na wapi uende bila kutumia Internet, pia utaweza kutumia kamera ya simu yako kuweza kuona sehemu halisi unapoenda moja kwa moja kupitia kwenye kamera ya simu yako. Pamoja na mengine mengi sana.

Kwa mujibu wa watumiaji wa dira hii kutoka nje ya nchi, dira hii ina lavel za kijeshi yani ni sawa na dira inayotumiwa na wanajeshi mbalimbali. Sina uhakika sana na hili ila unaweza kujaribu ili kujua kama dira hii ina uwezo unaosemwa.

Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini, baada ya kudownload install app kwenye simu yako kisha fungua app hii.

Download App Hapa

Ndani ya app utaweza kupata aina tatu za dira, kuna dira yenye kuonyesha muelekeo, dira ya ramani na dira ya kwenye kamera.

Utaweza kuwasha dira zote kwa kutumia vitufe vilivyoko chini ya app hii kama inavyoweza kuonekana kwenye picha hapo chini.

Kwa kufanya hivyo utakuwa umewezesha dira hii ya kisasa kwa urahisi kupitia simu yako ya Android. Kwa maoni yangu hii ni dira bora sana kati ya app zote za dira ambazo nimewahi kujaribu.

  • maujanja
  • maujanja ya android
Updated:
Previous Post
Jinsi ya Kuchukua Screenshot Kwenye Kompyuta
March 6, 2023
2 min read
Next Post

How to Apply for Passport in Tanzania (2026)

March 8, 2023
3 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Zuia Picha Zako Kuibiwa Kwenye Mitandao ya Kijamii
March 25, 2023
3 min read
  • Maujanja
Simu Yako Ina GB 64.? Ongeza Storage Kwa Kutumia Njia Hii
March 18, 2023
3 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine (Updated)
March 13, 2023
2 min read

Related guides