Huu Hapa Muonekano wa Giza Kwenye Programu ya WhatsApp

Kama wewe ni mfuatiliaji wa habari mbalimbali hapa VinkoWeb basi lazima utakuwa unajua habari kuhusu WhatsApp kuja na sehemu mpya ya Dark Mode au muonekano wa giza kwaajili ya kulinda macho yako wakati wa usiku. Sehemu h…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Kama wewe ni mfuatiliaji wa habari mbalimbali hapa VinkoWeb basi lazima utakuwa unajua habari kuhusu WhatsApp kuja na sehemu mpya ya Dark Mode au muonekano wa giza kwaajili ya kulinda macho yako wakati wa usiku.

Sehemu hii ni kama ile inayopatikana kwenye tovuti hii na app yetu ya VinkoWeb, sehemu hii itakusaidia kubadilisha muonekano wa tovuti nzima na kuwa na muonekano mweusi ambao huu ni mzuri zaidi kwaajili ya kulinda macho yako hasa wakati wa usiku. Sasa sehemu kama hii inakuja kwenye programu ya WhatsApp ambayo nayo pia itakupa nafasi ya kuweza kuwasha muonekano huo wa giza ili kuweza kulinda macho yako hasa unapokuwa unachati wakati wa usiku.

Kwa kuwa bado sehemu hii iko kwenye hatua ya majaribio, kupitia tovuti ya WAbetainfo tumefanikiwa kupata picha ambazo zina onyesha muonekano wa programu ya WhatsApp ikiwa sehemu hiyo ya Dark Mode au muonekano wa giza ukiwa umewashwa.

Kwa sasa, kama unataka kujua zaidi jinsi ya kulinda macho yako yasiharibiwe na mwanga wa vifaa vya kielektroniki kama vile simu na kompyuta, soma hapa kuhusu sheria ya 20 20 20 ambayo itasaidia kulinda macho yako hasa kama unatumia vifaa hivyo kwa muda mrefu.

Related guides

Related gadgets