Mwanamuziki Chamillionaire Azindua App Yake Mpya ya Convoz

Mwanamuziki ambae ni rapper wa zamani kidogo wa nchini marekani Chamillionaire, hivi karibuni amezindua App yake mpya inayoitwa Convoz. App hiyo mpya ambayo itahusiana na mitandao ya kijamii ni moja kati ya App ya tofaut…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read

Mwanamuziki ambae ni rapper wa zamani kidogo wa nchini marekani Chamillionaire, hivi karibuni amezindua App yake mpya inayoitwa Convoz. App hiyo mpya ambayo itahusiana na mitandao ya kijamii ni moja kati ya App ya tofauti sana.

Akiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa App hiyo, ambao pia ulikua mkutano wa wawekezaji na wajasiriamali, mwanamuziki Chamillionaire alitangaza kuhusu App hiyo mpya ya Convoz ambayo ita kuwa ikiunganisha watu mbalimbali kwa njia ya video kama ilivyo stories.

https://www.instagram.com/p/BXWQRuBFdqV/?utm_source=ig_embed

Lakini tofauti na Stories iliyopo kwenye App nyingi za sasa za mitandao ya kijamii, App ya Convoz inashirikisha mastaa na wasanii mbalimbali ambao unaweza kuongea nao moja kwa moja kupitia video ndani ya App hiyo.

Tofauti na kuchat kwa maneno ya kuandika, kupitia App hiyo mpya ya Convoz utaweza kuchati kwa kutumia video na ili kutumia app hiyo mtumiaji anakuwa na uwezo wa kurekodi video na kisha kuituma kwa msanii au mtu yoyote anaye mpenda alafu baadae msanii huyo hujibu meseji hiyo na yote hayo hufanyika kwa njia ya Video.

Kwa sasa App hii bado haija anza kupatikana rasmi Tanzania, lakini kupitia tamasha la uzinduzi wa App hiyo (Upfront Summit in Los Angeles), Chamillionaire ameahidi kufikisha App hiyo kila upande duniani na hii ni kutoa nafasi kwa watu kuweza kuongea na kuwaona wasanii na watu wanao wapenda.

The app was not found in the store. :-(

Related guides

Related gadgets