Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono

Amani JosephJuly 5, 20222 min read Ni wazi kuwa ni rahisi sana kubadilisha mwandiko wa mkono au mwandiko ulio andikwa kwa mkono kuwa mwandiko ulio andikwa na kompyuta, lakini je ulishawahi kujiuliza unawezaje kubadili mw…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
July 5, 2022
2 min read

Ni wazi kuwa ni rahisi sana kubadilisha mwandiko wa mkono au mwandiko ulio andikwa kwa mkono kuwa mwandiko ulio andikwa na kompyuta, lakini je ulishawahi kujiuliza unawezaje kubadili mwandiko ulio andikwa na kompyuta kuwa kama mwandiko ulioandikwa kwa mkono..?

Kama ulikuwa unajiuliza sana basi majibu yapo kwenye makala hii. Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kubadilisha mwandiko wa kompyuta kuwa mwandiko wa mkono.

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, hayo ni maandishi ambayo yameandikwa kwa kompyuta na kubadilshwa kuwa maandishi yaliyo andikwa kwa mkono. Mbali na maandishi pia utaweza kuweka maandishi hayo kwenye mistari kama ilivyo kwenye daftari kama unavyo ona kwenye picha hapo juu.

Basi bila kuendelea kupoteza muda mwingi moja kwa moja twende kwenye hatua hizi muhimu. Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload unaweza kuzima data kwenye simu yako moja kwa moja kisha ndio ufungue app hii, hiyo inasaidia kwa kuwa app hii ina matangazo mengi sana lakini pia inaweza kufanya kazi bila Internet.

Baada ya kufungua app hii bofya sehemu ya Create New iliyopo chini upande wa kulia

Baada ya hapo utaletewa ukurasa mpya kisha bofya kwenye ukurasa huo kufungua.

Baada ya hapo utaletewa ukurasa mpya ambao unaweza kutumia kuandika maandishi yalio andikwa kwenye kompyuta na kuyabadilisha kuwa mwandiko ulio andikwa na mkono.

Kwenye ukurasa huu unaweza kupaste maandishi yoyote ambayo ume copy kutoka sehemu yoyote hii ni rahisi kwa mwanafunzi au mtu yoyote ambaye anataka kuandika maandishi kwa haraka kutoka kwenye mfumo wa kuchapisha kuja kwenye mfumo wa mwandiko wa mkono.

Kwa kufanya hivyo natumaini utakuwa umeweza kubadilisha mwandiko wa kompyuta kuwa mwandiko wa mkono. Njia hii ni bora na inaweza kusaidia sana wanafunzi hasa pale ambapo unataka kuandika assgment ambayo ni lazima iandikwe kwa mkono.

Kupitia app hii unaweza kuweka maandishi kwenye PDF ambapo utaweza kuprint maandishi hayo kwa urahisi kupitia app hii au kwa kutuma file hilo la PDF.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Simu Bora za Samsung Galaxy A Series (Updated 2026)
July 3, 2022
1 min read
Next Post

Best iPhones (2026 Updated)

July 6, 2022
1 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Jinsi ya Kubadilisha Picha Kuwa Video ya Muda Mfupi
July 15, 2022
2 min read
  • Maujanja
Ongeza Ukubwa, Ngarisha Picha Bila Kupoteza Ubora (Android)
July 14, 2022
2 min read
  • Maujanja
Fahamu Mambo Haya Muhimu Kuhusu Password Yako
July 12, 2022
4 min read

Related guides

Related gadgets