Hatimaye Kampuni ya Airtel Tanzania Kuwezesha Mtandao wa 4G

Baada ya kampuni za kutoa huduma za simu za Vodacom Tanzania na Tigo Tanzania kuwezesha mtandao wa 4G nchini Tanzania, hatimaye baada ya takribani miaka mitatu kampuni ya kutoa huduma za simu ya Airtel Tanzania nayo inat…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Baada ya kampuni za kutoa huduma za simu za Vodacom Tanzania na Tigo Tanzania kuwezesha mtandao wa 4G nchini Tanzania, hatimaye baada ya takribani miaka mitatu kampuni ya kutoa huduma za simu ya Airtel Tanzania nayo inategemea kuwezesha huduma hiyo ya 4G kwa wateja wake hivi karibuni.

Kwa mujibu ya maelezo ya mmoja wa watoa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania, huduma hiyo kwa sasa ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilika na watumiaji wa mtandao huo wa simu kwa sasa wanapaswa kubadilisha laini zao ili kuwezesha mtandao 4G kwenye laini zao ili mtandao huo utakapo wezeshwa waweze kupata huduma hiyo moja kwa moja.

Hata hivyo kwa sasa kama unayo laini ya simu ya Airtel Tanzania, unaweza kuangalia kama simu yako pamoja na laini kama zina uwezo wa 4G kwa kubofya *149*95#. Kama laini yako pamoja na simu vyote vinayo uwezo wa 4G basi endelea kusubiria pale utakapo pata ujumbe wa huduma hiyo kuanza kutumika. Kama laini yako haina huduma hizo basi unashauriwa kufika kwenye maduka ya airtel yaliyopo karibu na wewe ili kujua hatua za kufuata.

Related guides

Related gadgets